• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Russia wakutana Moscow

    (GMT+08:00) 2019-06-06 08:50:25

    Rais Vladimir Putin wa Russia amekutana na mwenzake Xi Jinping wa China katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow.

    Viongozi hao wamepongeza maendeleo ya uhusiano wa nchi mbili katika miaka 70 iliyopita, na kukubaliana kuendeleza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya pande hizo mbili katika zama mpya ufikie ngazi ya juu, ili kunufaisha watu wa nchi hizo mbili na dunia kwa ujumla.

    Rais Xi Jinping amesema, nchi hizo mbili zinapaswa kuimarisha ushirikiano na mawasiliano ya kimkakati, na kuungana mkono zaidi katika masuala yanayohusiana na maslahi makuu ya upande mwingine. Ameongeza kuwa China na Russia zitaendelea kulinda mfumo wa biashara ya pande nyingi, kutia nguvu chanya ya msukumo kwenye mazingira ya kimataifa yenye utatanishi, na kutoa mchango mpya katika kujenga Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Kwa upande wake rais Putin amesema uhusiano wa wenzi wa kimkakati uliojengwa kihalisi kati ya nchi hizo mbili si kama tu umenufaisha watu wa pande hizo mbili, na pia umekuwa nguvu muhimu ya kulinda usalama wa kimataifa na utulivu wa kimkakati duniani. Amesema Russia na China zinapaswa kuendelea kuimarisha ushirikiano na uratibu katika masuala makubwa ya kimataifa na ya kikanda, ili kukabiliana kwa pamoja changamoto zinazotokana na hatua za upande mmoja na sera za kujilinda kibiashara, na kulinda amani na utulivu duniani.

    Baada ya mazungumzo, marais hao walisaini Taarifa ya pamoja kuhusu kuendeleza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi zao katika zama mpya, na Taarifa ya pamoja kuhusu kuimarisha utulivu wa kimkakati duniani, na kushuhudia kusainiwa kwa nyaraka nyingine za ushirikiano wa pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako