• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TBS yatoa mafunzo ya ubora wa bidhaa

    (GMT+08:00) 2019-06-06 18:48:10
    Shirika la viwango nchini Tanzania (TBS) limeanza kutoa elimu ya ubora wa bidhaa kwa wazalishaji na wenye viwanda vidogo na vikubwa ili kuwezesha bidhaa zao kukidhi matakwa ya kisheria na soko la ndani nan je.

    Ofisa Uhakiki Ubora kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam,Stella Mroso amesema leno la elimu hiyo ni kuhakikisha bidhaa zinzalishwa katika ubora unaotakiwa.

    Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini ambayo ni Njombe,Iringa,Mbeya,Songwe,Rukwa na kuwa wamepewa elimu na TBS ya mifumo ya uongozi katika masuala ya ubora na mfumo ili waweze kukidhi viwango vya ubora vya kimataifa.

    Alisema hadi sasa wazalishaji zaidi ya 300 kutoka mikoa sita nchini humo wamepatiwa mafunzo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako