• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Russia zina majukumu na wajibu wa kulinda utulivu wa kimkakati duniani

    (GMT+08:00) 2019-06-06 19:57:55

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China na Russia zikiwa ni wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zina majukumu na wajibu wa kulinda utulivu wa kimkakati duniani. Taarifa ya pamoja iliyotolewa na kusainiwa na viongozi wa nchi hizo mbili kuhusu kuimarisha utulivu wa kimkakati duniani, imeonesha nia thabiti ya nchi hizo mbili katika kulinda utaratibu wa pande nyingi wa kimataifa.

    Bw. Geng ameeleza kuwa taarifa hiyo imesisitiza umuhimu wa kulinda uhusiano mzuri kati ya nchi kubwa kwa utatuzi wa masuala ya kimkakati duniani, na kutangaza hatua halisi katika kuimarisha utulivu wa kimkakati na kulinda udhibiti wa silaha, na utaratibu wa kimataifa katika kuzuia kuene kwa silaha za kemikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako