• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 61 wauawa katika matukio ya kiusalama nchini Sudan

    (GMT+08:00) 2019-06-07 09:00:20

    Serikali ya Sudan imesema watu 61 wameuawa nchini humo kutokana na matukio ya kiusalama.

    Msaidizi wa waziri wa afya wa nchi hiyo Suleiman Abdul Jabbar amesema, idadi ya watu waliouawa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum ilifikia 52, na wengine tisa waliuawa katika matukio ya kiusalama kwenye mikoa mingine mitatu ya nchi hiyo.

    Wakati huohuo, Umoja wa Afrika umeeleza kulaani mauaji ya raia nchini Sudan, na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyike kuhusu matukio hayo.

    Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Amani na Usalama ya Umoja huo imesema, Umoja huo umelaani vifo vya watu wasio na hatia, na kutaka uchunguzi huru ufanyike juu ya matukio hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako