Mwendesha mashtaka mkuu wa Rwanda Jean Mutangana ameihimiza Burundi kushughulikia watu waliohusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi. Hadi sasa, Burundi haijawafikisha karibu watu 6,000 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo mbele ya sheria. Mutangana amesema Rwanda inafikiria kushirikiana na polisi wa kimataifa (Interpol) kuwakamata watu hao watakapotoka nje ya nchi yao. Mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 yalisababisha vifo vya watu karibu milioni moja, wengi wao wakiwa ni watutsi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |