• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa afya wa Kenya avilaumu viwanda kwa kutengeneza vyakula visivyo na ubora

    (GMT+08:00) 2019-06-08 17:26:55

    Waziri wa afya wa Kenya Sicily Kariuki jana alivitupia lawama viwanda vinavyotengeneza mafuta yasiyo salama kwa afya, vyakula vyenye chembe za sumu na uwepo wa mabaki ya dawa kwa bidhaa zisizo na ubora.

    Akiongea kwenye mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Usalama wa Chakula Duniani mjini Nairobi, Bi Kariuki amesema uwepo wa mabaki ya dawa kwenye mifugo na chakula kutokuwa na ubora pia ni masuala yanayoipa wasiwasi serikali. Aidha amewahimiza wazalishaji kuzalisha chakula salama, wasafirishaji kuhakikisha chakula kinakuwa salama na watengenezaji kuzalisha bidhaa salama na zenye lishe ili kuwawezesha wanunuzi kupata chakula salama na chenye ubora.

    Amesisitiza kuwa Kenya inatilia mkazo usalama wa chakula kwa vile imekuwa ikitambua kuwa ni nguzo muhimu ya kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako