• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China asema ziara ya rais Xi Jinping nchini Russia yaimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2019-06-08 17:28:02

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana alisema, ziara ya rais Xi Jinping wa China nchini Russia imeonyesha ishara kwamba, makubaliano kati ya China na Russia ya kuzidisha ushirikiano wa kuaminiana ni imara, na nia ya China ya kupendekeza ushirikiano wa kunufaishana ni imara, inaimarisha uhusiano kati ya nchi kubwa, inatia uhai kwa maendeleo ya dunia nzima na kutia nguvu kwa jumuiya ya kimataifa.

    Bw. Wang Yi amesema, wakuu wa nchi hizo mbili wamefanya mazungumzo na kusaini taarifa ya pamoja kutangaza kuendeleza uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Russia katika zama mpya na kutimiza maendeleo yenye sifa bora ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kuwa ni matokeo makubwa ya kisiasa ya ziara hiyo.

    Amesema, hali imeonyesha kuwa mshikamano na ushirikiano kati ya China na Russia vinaendana na maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili na jumuiya ya kimataifa, nchi hizo mbili hazilengi upande wa tatu, pia hazitachochewa na kuingiliwa na upande wa tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako