• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Mapendekezo ya China" yasaidia dunia kuanzisha njia mpya ya maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2019-06-08 18:51:07

    Rais Xi Jinping wa China jana alihudhuria mkutano wa baraza la uchumi la kimataifa la St. Petersburg, na kutoa hotuba ya "kushikilia maendeleo endelevu, kujenga kwa pamoja dunia nzuri yenye ustawi", ambapo ametoa mapendekezo matatu ya kushirikiana kujenga uchumi wa dunia wa aina mbalimbali, kujenga jamii yenye furaha na manufaa, na kujenga makazi mazuri ya kuishi binadamu na maumbile pamoja kwa masikilizano. Rais Xi ametoa mapendekezo ya China kwa dunia kuanzisha njia mpya ya maendeleo endelevu.

    Mkutano wa mwaka huu wa baraza la uchumi la kimataifa la St. Petersburg unafuatilia ajenda ya maendeleo endelevu. Rais Xi ameeleza mapendekezo ya China kuhusu majukumu matatu ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa na kutoa mawazo na nishati kwa jumuiya ya kimataifa kuimarisha ushirikiano wa maendeleo.

    Hotuba ya rais Xi imeinua kwa nguvu imani ya jumuiya ya kimataifa kwa maendeleo endelevu ya China na dunia nzima. Kwa mfano, rais Vladmir Putin wa Russia amesema utaratibu wa kimataifa usio wa haki hautakuwa imara na endelevu, inafaa kujadili utaratibu mpya wa kimataifa juu ya msingi wa makubaliano ya jumuiya ya kimataifa, kuheshimu hadhi ya kiini ya Umoja wa Mataifa katika mambo ya kimataifa, na kuzingatia ipasavyo maslahi ya maendeleo ya nchi zinazoendelea. Viongozi wengine wanaohudhuria mkutano huo pia wamesema ili kukabiliana na masuala na michakato mbalimbali inayoikabili jamii ya binadamu, nchi mbalimbali zinapaswa kushirikiana. Pia zinaona kuwa, China imekuwa nguvu kubwa ya kulinda hali yenye pande nyingi, kanuni ya kimataifa na biashara huria.

    China imetoa mchango mkubwa kwa ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa katika kuhimiza maendeleo endelevu ya uchumi, jamii na mazingira. China inaona kuwa, maendeleo endelevu ni ufunguo wa dhahabu wa kutatua masuala ya dunia. Kwa kupitia hotuba ya rais Xi, jumuiya ya kimataifa inaamini zaidi kuwa China itaendelea kushiriki kwenye mchakato wa maendeleo ya dunia na kufanya mambo yake yenyewe, ili kuhimiza dunia kuanzisha njia mpya ya maendeleo endelevu, na kuchangia busara ya China na kutia nguvu ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako