• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yasema Sudan kusimamishwa uanachama wa AU hakutaathiri mchakato wa amani wa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-06-09 17:42:38

    Sudan Kusini yasema Sudan kusimamishwa uanachama wa Umoja wa Afrika hakutaathiri makubaliano ya amani ya mwezi Septemba mwaka 2018, ambayo Sudan ulikuwa mdhamini.

    Waziri wa habari wa Sudan Kusini ambaye pia ni msemaji wa serikali ya nchi hiyo Bw. Michael Makuei amesema Sudan kusimamishwa uanachama wa Umoja wa Afrika kutakuwa na athari ndogo katika utekelezaji wa makubaliano, kwa kuwa IGAD inaendelea kuongoza juhudi za amani nchini Sudan Kusini.

    Sudan imesimamishwa uanachama wa Umoja wa Afrika baada ya vurugu kutokea alhamisi katika mji mkuu wake Khartoum, na kusababisha vifo vya waandamanaji wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako