• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wataka nchi za nje zisiingilie kati mambo ya ndani ya Sudan

    (GMT+08:00) 2019-06-09 17:47:34

    Umoja wa Afrika umezitaka nchi za nje zisiingilie mambo ya ndani ya Sudan wakati nchi hiyo ikiwa njia panda kutokana na kuwepo kwa sintofahamu ya kisasa.

    Mwito huo umetolewa na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Mousa Mahamat kwenye taarifa iliyotolewa leo, akisisitiza haja ya kutafuta suluhisho linaloongozwa na Sudan kwenye msukosuko wa kisiasa unaendelea nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti huyo inasema pande mbalimbali zinatakiwa kuunga mkono juhudi za Umoja wa Afrika kuunga mkono mchakato unaoongozwa na wasudan, na kuheshimu nia na matakwa ya wananchi wa Sudan.

    Bw. Mahamat pia amezihimiza pande mbalimbali nchini Sudan kuchukua hatua zote muhimu za kisiasa na kiusalama kuweka njia ya kurudisha mazungumzo na kufikia makubaliano ya kurudi kwenye serikali ya kiraia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako