• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Warundi waandamana kupinga ripoti za baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa inayoichafua nchi yao

    (GMT+08:00) 2019-06-09 17:51:18

    Wananchi wa Burundi wamefanya maandamano katika nchi nzima kupinga baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa "kuchafua" sura ya Burundi, na kuvilaumu baadhi ya vyombo vya habari vya Ufaransa.

    Maandamano hayo yanatokana na ripoti ya mahojiano yaliyofanyika tarehe 2 Juni kati ya mwanaharaki Marguirite Barankitse ambaye anaishi uhamishoni nchini Ufaransa tangu mwaka 2015, na Radio ya Ufaransa RFI.

    Mwenyekiti wa baraza la vyombo vya habari la Burundi Bw. Nestor Bunkumukunzi amesema mahojiano hayo hayakuwa na usawa, na yamekiuka sheria ya habari. Amesema mhojiwa alikuwa nia ya wazi ya kuchafua sura ya Burundi kwa uongo, matusi makubwa na kumchafua kiongozi wa Burundi.

    Waandamanaji walikuwa na mabango yanayosema jumuiya za kiraia zinapinga tabia ya baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa, hasa vya Ufaransa, kuwaunga mkono waliojaribu kufanya mapinduzi mwaka 2015 na washirika wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako