• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Malawi akana madai ya upinzani ya kuiba kura katika uchaguzi

    (GMT+08:00) 2019-06-10 08:51:39

    Rais mpya wa Malawi Bw. Peter Mutharika amelaani upinzani akisema hakuhusika na wizi wa kura katika uchaguzi wa rais uliofanyika Mei 21, na kwamba Wamalawi ndio waliomchagua.

    Rais Mutharika amesema hayo mjini Blantyre katika mkutano wake wa kwanza wa kisiasa tangu alipoapishwa Mei 27 na kuingia madarakani rasmi Mei 31, kufuatia viongozi wa upinzani kudai kuwa wizi wa kura ulimsaidia Mutharika kushinda katika uchaguzi huo.

    Rais Mutharika ameushutumu upinzani kuiba kura zake katika mkoa wa kati na kusema kuwa uchunguzi unaendelea. Pia amemtuhumu kiongozi wa chama cha MCP Bw. Lazarus Chakwera kwa kuchochea vurugu, ambapo wafuasi wa chama hicho waliharibu miundombinu katika maandamano yao ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako