• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China kufanya ziara katika Asia ya kati na kuhudhuria mkutano wa SCO na mkutano wa CICA

  (GMT+08:00) 2019-06-10 17:00:48

  Rais Xi Jinping wa China atafanya ziara rasmi nchini Kyrgyzstan na Tajikistan kuanzia tarehe 12 hadi 16, na kuhuduria mikutana kadhaa mikubwa itakayofanyika katika nchi hizo ukiwemo mkutano wa 19 wa kamati ya utendaji ya viongozi ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zhang Hanhui amesema, ziara hiyo itasukuma mbele uhusiano kati ya China na nchi hizo mbili za Asia ya kati.

  Kyrgyzstan na Tajikistan ni nchi jirani na China, na China imedumisha maendeleo mazuri ya uhusiano kati yake na nchi za Asia ya kati zikiwemo nchi hizo mbili. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zhang Hanhui amesema, ziara hiyo itahimiza uhusiano kati ya China na nchi hizo mbili kupata maendeleo zaidi. Anasema,

  "Rais Xi pamoja na viongozi wa Kyrgyzstan na Tajikistan watatoa mpango mpya kuhusu mustakabali wa uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na nchi hizo mbili, na kuimarisha zaidi msingi wa kisasa kwa maendeleo ya uhusiano huo. Aidha, watatoa mpango mpya kuhusu ushirikiano wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', ili kuboresha maisha ya watu na kuhimiza maendeleo ya nchi hizo."

  Rais Xi atahudhuria mkutano wa 19 wa kamati ya utendaji ya viongozi ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) utakaofanyika mjini Bishkek nchini Kyrgyzstan. Bw. Zhang anasema, mkutano huo utajadili hali ya sasa na mustakabali wa SCO na masuala muhimu ya kimataifa na kikanda. Rais Xi atabadiliana maoni na viongozi wa nchi mbalimbali watakaohudhuria mkutano huo kuhusu masuala hayo, na kujadili mawazo na hatua mpya za kushirikiana ili kukabiliana na changamoto, na kuhimiza amani, utulivu, maendeleo na ustawi.

  Bw. Zhang amesema, katika miaka 18 iliyopita tangu kuanzishwa kwake, jumuiya hiyo imeimarisha uaminifu na ushirikiano katika sekta mbalimbali, kushiriki kwenye masuala ya kikanda na kimataifa kwa hatua madhubuti, na kufanya kazi muhimu za kiujenzi kwa ajili ya kuhimiza amani na mendeleo ya kikanda, na kulinda haki ya kimataifa. Anasema,

  "Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai imepongezwa na jumuiya ya kimataifa kwa kulinda usalama na utulivu wa kikanda na kuhimiza maendeleo ya nchi wanachama wake. China inaamini kuwa pande husika zitachukua mkutano wa Bishkek kama fursa nzuri ya kukusanya maoni ya pamoja na kufikia makubaliano ya ushirikiano, ili kuhimiza jumuiya hiyo kupata maendeleo mapya."

  Rais Xi pia atahudhuria mkutano wa mkutano wa tano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano na Hatua za Kujenga Uaminifu Barani Asia CICA utakaofanyika mjini Dushanbe nchini Tajikistan. Bw. Zhang amesema katika miaka 27 iliyopita tangu kuanzishwa, baraza hilo limetoa mchango chanya kwa ajili ya kuhimiza mawasiliano, uaminifu na ushirikiano kati ya pande husika. Anasema,

  "Kauli mbiu ya mkutano huo ni 'matarajio ya pamoja, kwa ajili ya Asia yenye usalama na ustawi zaidi'. China itapendekeza kuendelea kutekeleza mawazo endelevu ya pamoja ya usalama, jumla na ushirikiano, kutokana na maendeleo na mabadiliko mapya ya kikanda."

  Bw. Zhang amesisitiza kuwa anaamini ziara ya rais Xi itapata mafanikio makubwa kutokana na juhudi za pande mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako