• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mawaziri wa biashara na uchumi wa kidigitali wa kundi la nchi 20 wasisitiza kuhimiza mageuzi ya shirika la biashara la dunia

    (GMT+08:00) 2019-06-10 19:37:10

    Mkutano wa mawaziri wa biashara na uchumi wa kidigitali wa nchi za kundi la nchi 20 ulifunguliwa jana huko Tsukuba, nchini Japan. Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo imesema ni muhimu sana kulinda mazingira ya uhuru na usawa wa kibiashara, na kundi la nchi 20 linapaswa kufanya juhudi kuhimiza mageuzi ya shirika la biashara la dunia.

    Taarifa hiyo imesema kundi la nchi 20 linapaswa kuchukua hatua kuimarisha mfumo wa utatuzi wa mgogoro wa shirika la biashara la dunia. Pia imesema kupanua biashara na uwekezaji ni muhimu katika kuhimiza ustawi wa uchumi na ongezeko la kudumu, lakini tishio la mazingira ya biashara la hivi sasa huenda litasababisha kupungua kwa ongezeko la uchumi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako