• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania and Uganda zimesitisha ubadilishaji wa noti za Kenya

    (GMT+08:00) 2019-06-10 19:43:12

    Benki ya Tanzania imesimamisha ubadilisha wa noti za Kenya.

    Kupitia barua iliyoelekezwa kwa taasisi zote za kifedha siku ya Ijumaa, mdhibiti wa benki ya Tanzania amesema Benki Kuu ya Kenya imeihakikishia utumizi wa noti mpya kuanzia Mei 31.

    Kwa lengo la kupambana na fedha bandia nchini Kenya, Benki ya Tanzania imeshauriwa kusimamisha ubadilishaji wa fedha mara moja.

    Hii inamaanisha, mtu yeyote aliye na noti ya zamani katika hizi mbili Tanzania na Uganda basi atalazimika kuzileta nchini kubadilisha na zile mpya agizo kutoka kwa Benki Kuu ya Kenya CBK

    Tangazo ni pigo kwa wahusika ambao wamepeleka kiasi kikubwa cha fedha za Kenya katika mataifa jirani, wakitarajia kubadilisha pesa bandia kwa sarafu ya nchi hizo.

    Pia ni pigo kubwa kwa wafanyabiashara wa Kenya wanaotaka kubadilishana fedha za biashara Tanzania na Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako