• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China waendelea vizuri licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali

    (GMT+08:00) 2019-06-10 19:52:45

    Takwimu zilizotolewa leo na idara kuu ya forodha ya China zinaonesha kuwa, katika miezi mitano iliyopita mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje imefikia karibu dola za kimarekani trilioni 1.76, ambalo ni ongezeko la asilimia 4.1 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

    Wakati mivutano ya kibiashara inaongezeka duniani, biashara kati ya China na nchi za nje bado inaendelea kwa utulivu. Hali hii inaonesha kuwa uchumi wa China una nguvu kubwa ya kuendelea, na kuweza kuhimili changamoto yoyote.

    Ingawa biashara kati ya China na Marekani ilipungua kwa asilimia 9.6 katika miezi mitano iliyopita, lakini biashara kati ya China na Umoja wa Ulaya, Umoja wa Nchi za Kusini mwa Asia na Japan iliendelea kuongezeka, haswa thamani ya biashara kati ya China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" iliongezeka kwa asilimia 9. Hali hii inaonesha kuwa China ina uwezo wa kurekebisha muundo wake wa biashara kutokana na mgongano wa kibiashara kati yake na Marekani.

    Kutoka msukosuko wa fedha barani Asia wa mwaka 1997 hadi msukosuko wa fedha duniani wa mwaka 2008, uchumi wa China umeimarika zaidi baada ya kushinda changamoto. Ikiwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi na nchi ya kwanza kwa ukubwa wa viwanda, pato la taifa la China limezidi dola za kimarekani trilioni 13, na pia China ina soko kubwa la watu bilioni 1.4. Hivyo China ina uwezo wa kutosha katika kukabiliana na changamoto yoyote.

    Uchumi wa China pia umekuwa injini ya uchumi wa dunia. Katika miaka kadhaa iliyopita China imechangia asilimia 30 ya ongezeko la uchumi wa dunia. Shirika la Ushirikiano wa Uchumi Duniani linakadiria kuwa, China itaendelea kuwa nchi inayochangia zaidi ongezeko la uchumi wa dunia kwa muda mrefu.

    Ingawa mvutano wa kibiashara uliochochewa na Marekani umeleta changamoto kwa uchumi wa China, lakini China inaitambulisha dunia kuwa, hali nzuri ya maendeleo ya uchumi wake haibadiliki, na itaendelea kusukuma mbele mageuzi na kufungua mlango, ili kufanya vizuri mambo yake yenyewe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako