• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TENISI: Nadal abeba taji la 12 michuano ya wazi ya tenisi ya Ufaransa

  (GMT+08:00) 2019-06-11 08:33:53

  Rafael Nadal hakamatiki kwenye michuano ya wazi ya tenisi ya Ufaransa baada ya kumchapa Dominic Thiem na kubeba taji la 12 la mashindano hayo kwa upande wa wanaume.

  Mhispania huyo alishinda taji hilo la Grand Slam kwa mwaka wa tatu mflulizo huko Roland Garros baada ya kumtandika Thiem kwa seti 6-3, 5-7, 6-16 na 6-1 katika fainali iliyokuwa na upinzani mkali.

  Taji hilo ni la 18 katika historia yake ya kunyakua mataji makubwa kwenye mchezo huo tangu aanze kucheza, huku akiwa amezidiwa na mataji mawili tu na Mswidishi Roger Federer, upande wa michuano ya wazi ya Ufaransa, Nadal amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda taji hilo mara 12.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako