• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa msaada wa dharura wa chakula kwa Kenya

    (GMT+08:00) 2019-06-11 17:08:09

    Balozi wa China nchini Kenya Bw. Wu Peng jana alitangaza kuwa, serikali ya China imetoa msaada wa chakula wenye thamani ya dola milioni 11.6 za kimarekani kwa Kenya, ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na ukame ambao ni mbaya zaidi tangu miaka 38 iliyopita.

    Kenya imekumbwa na ukame ambao ni mbaya zaidi tangu miaka 38 iliyopita, na watu milioni 1.1 wa kaunti zaidi ya 10 hususani Turkana wanahitaji msaada wa chakula. Balozi wa China nchini Kenya Bw. Wu Peng amesema, serikali ya China imeamua kutoa msaada wa mchele tani 11,835 wenye thamani ya dola milioni 11.6 za kimarekani. Anasema,

    "Shehena ya kwanza imefika mjini Mombasa tarehe 19, Mei, na chakula kimeanza kutolewa kwa watu walioathiriwa na ukame. Shehena ya pili ya chakula tani 1,500 itasafirishwa mwishoni mwa mwezi huu. ubalozi wa China unashirikiana na idara husika za Kenya kwa karibu, ili kuhakikisha chakula kinafikishwa kwa watu walioathiriwa kwa haraka."

    Hii sio mara ya kwanza ya China kutoa msaada wa chakula kwa Kenya. Mwaka 2011 na mwaka 2017, China ilitoa misaada ya chakula yenye thamani ya dola milioni 18.9 na 21.8 za kimarekani kwa mamilioni ya wakenya waliokumbwa na ukame. Waziri wa mpangilio wa madaraka wa Kenya Bw. Eugene Wamalwa amesema, mwaka 2017 watu milioni tatu nchini Kenya waliathiriwa na ukame, na msaada wa chakula uliotolewa na China uliwasaidia sana. Anasema,

    "Kila tunapokabiliwa na changamoto, tunasema mtu anayetupa uungaji mkono ni rafiki kweli. Kuanzia mwezi Julai mwaka huu, tutakabiliwa tena na ukame wa kutisha, na idadi ya kaunti zinazoathiriwa inaweza kuongezeka. Tumepata magunia zaidi ya elfu 10 ya mchele kutoka Kenya, ambayo yamegawanywa kwa kaunti 17."

    Bw. Wu amesema, tangu Kenya ipate uhuru, China imetoa misaada kwa miradi karibu 100 ya Kenya katika sekta za miundombinu, afya, elimu, kilimo, nguvukazi, nishati, uhifadhi wa mazingira na hali ya kibinadamu, ili kuhimiza maendeleo ya jamii na uchumi na kuboresha maisha ya watu nchini Kenya. Ameongeza kuwa, ikiwa mwenzi muhimu wa kimaendeleo wa Kenya, China itatoa misaada kwa kulingana na "ajenda nne kuu" za Kenya, haswa sekta ya uzalishaji. Anasema,

    "Serikali ya nchi hizo mbili zinafanya ushirikiano wa kutoa mafunzo ya kazi kwa walimu wa Kenya, na walimu hao watakuwa "mbegu" wa kutoa mafunzo ya ajira nchini Kenya, ili kuwasaidia watu kupata ajira na kuongeza kipato. Tunatumai mbegu hizo zitakua na kuwa miti mirefu, ambayo itanufaisha maendeleo ya Kenya na uhusiano kati ya China na Kenya."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako