• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani haipaswi kuhusisha mambo yote na usalama wake

    (GMT+08:00) 2019-06-11 19:24:30

    Marekani imeweka alama ya "matishio ya usalama" ya nchi hiyo kwa bidhaa za chuma, aluminum, magari na vipuri vya magari kutoka nchi za nje, uwekezaji wa nje, wanafunzi na wasomi wa kigeni na hata akaunti za mitandao ya kijamii ya watu wanaoomba visa ya Marekani. Inaonekana kuwa Marekani inaweza kuhusisha mambo yoyote na usalama wake.

    Kufuatia maoni ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa, usalama wa taifa unamaanisha hali ya kutokuwepo matishio dhidi ya mamlaka, ukamilifu wa ardhi, neema ya wananchi, maendeleo endelevu ya uchumi na jamii, na maslahi mengine muhimu ya nchi. Lakini hivi sasa usalama wa taifa unatumiwa ovyo na Marekani ambayo ni nchi yenye nguvu zaidi duniani, kwa lengo la kujilinda kibiashara na kufanya vitendo vya umwamba dhidi ya nchi nyingine.

    Takwimu zinaonesha kuwa, kuanzia miaka ya 80 ya karne iliyopita hadi mwanzoni mwa karne hii, Marekani ilifanya "uchunguzi wa 232" mara 14, na kwa mara mbili tu ilitekeleza hatua ya kutoa adhabu. Lakini tangu mwaka 2017, Marekani inaonekana kuwa na wasiwasi kuhusu usalama wake, na kufanya "uchunguzi wa 232" mara nyingi, hususan ilitangaza "hali ya hatari " mwezi Mei mwaka huu. Ni kweli nchi nyingine zinaweza kutishia usalama wa Marekani ambayo ina nguvu kubwa zaidi duniani katika mambo ya jeshi, sayansi na teknolojia na uchumi?

    Ukweli ni kwamba, Marekani inataka kupata maslahi zaidi kutoka biashara kati yake na nchi nyingine kwa kisingizio cha "usalama wa taifa". Pia haikubali mabadiliko ya hali ya dunia kutokana na maendeleo ya nchi zinazoendelea. Kitendo hiki cha Marekani si kama tu kimedhuru maslahi ya wenzi wake wa kibiashara, bali pia kimeathiri utaratibu wa kimataifa na uaminifu wa nchi nyingine. Licha ya hayo, pia kinaweza kuifanya Marekani ikose uwezo wa kutambua matishio ya kweli dhidi ya usalama wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako