• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini imesema jeshi la pamoja litaundwa kutokana na fedha kuwepo

    (GMT+08:00) 2019-06-11 19:45:45

    Sudan Kusini imesema inapata maendeleo kwenye kuunda kambi na kuunganisha majeshi kutokana na kuwepo kwa fedha.

    Mkuu wa kamati ya pamoja ya kusimamisha vita Bw. Charles Madut Akol amesema kazi yao inaungwa mkono na dola milioni mbili ambazo zitasaidia kwa ajili ya maslahi ya wanajeshi, ambao wako tayari kukaguliwa kabla ya kuingia kambini.

    Amesema mwanzoni walikuwa wanakwamishwa na ukosefu wa fedha, lakini kazi inaendelea baada ya kutolewa kwa dola milioni mbili, na kamati ya mpito ya taifa. Kamati ya kusimamia usimamishaji wa vita pia imewapatia maduka ya kuhama ambayo ni makontena yanayoweza kutumika kuhifadhia vitu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako