Wizara ya usafiri ya China imesema vijiji vyote vya China vinatarajiwa kuwa na huduma ya usafiri wa mabasi kabla ya kufikiwa mwezi Septemba mwaka 2020.
Kwa sasa usafiri huo umefika kwenye asilimia 98.02 ya vijiji vyote, baada ya vijijini 2,944 kupata huduma hiyo tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na vijiji 1,698 vya maeneo maskini.
Msemaji wa wizara ya usafiri Bw. Wu Chungeng amesema vijiji zaidi ya elfu saba vilianza kupata huduma hiyo kila mwaka katika miaka mitano iliyopita, na kutoa ajira mfululizo. Hata hivyo mpaka sasa kuna vijiji elfu 16 ambavyo bado havina huduma ya usafiri wa mabasi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |