• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa watoa wito wa kumaliza vurugu nchini Sudan

    (GMT+08:00) 2019-06-12 09:34:36

    Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutokomeza vurugu nchini Sudan na kurejesha mazungumzo kati ya waandamanaji na Baraza la Mpito la Kijeshi (TMC).

    Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, wanafuatilia hali inavyoendelea nchini Sudan, na kutumai mazungumzo ya kisiasa yataanza tena. Ameongeza kuwa, mamlaka husika zinapaswa kuacha kukamata na kuzuia watu ambao wana nafasi kubwa katika mazungumzo hayo, na pia kurejesha huduma za mtandao wa internet na njia nyingine za mawasiliano.

    Dujarric pia ametoa wito kwa pande zote husika kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha kipindi cha amani cha mpito kinachoongozwa na raia na amani endelevu nchini kote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako