• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Nike watishia kusitisha mkataba na Neymar Jr.

    (GMT+08:00) 2019-06-12 09:47:39

    Kampuni ya vifaa vya michezo duniani Nike, imetishia kujitoa udhamini wake kwa nyota wa soka wa timu ya taifa Brazil na klabu ya PSG Neymar Jr kwa tuhuma za ubakaji.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, anakabiliwa na kesi ya ubakaji ambapo wiki iliyopita alifikishwa kituo cha polisi cha Sao Paulo nchini humo kujibu mashtaka baada ya mrembo Najila Trindade Mendes de Souza kuweka wazi kupitia kituo cha runinga cha SBT.

    Neymar alidaiwa kufanya tukio hilo Mei 15, katika hoteli ya Sofitel, iliopo Paris nchini Ufaransa, lakini mwana soka huyo alikanusha vikali huku akidai ni mipango ya kutaka kumpoteza katika soka.

    Nike ni moja kati ya kampuni ambazo zina mikataba na wachezaji wakubwa duniani, imekuwa ikivunja mikataba kwa wachezaji kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji, tuhuma za kutumia dawa za kulevya na mambo mengine ambayo hayatakiwi kwa jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako