• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Urari mbaya wa biashara ya huduma wa China wapungua

  (GMT+08:00) 2019-06-12 16:32:41

  Takwimu zilizotolewa leo na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, kuanzia mwezi Januari hadi Aprili mwaka huu, thamani ya biashara ya huduma kati ya China na nchi za nje ilizidi dola bilioni 253 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 4.1 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, na urari mbaya wa biashara ya huduma ulipungua kwa asilimia 9.7.

  Naibu mchunguzi wa idara ya biashara ya huduma ya wizara ya biashara ya China Bw. Zhu Guangyao ameeleza kuwa, katika miezi minne ya kwanza ya mwaka huu, huduma ya kiujuzi imeendelea vizuri. Anasema,

  "Kutokana na maendeleo ya mageuzi ya muundo wa utoaji na ongezeko la uwezo wa ushindani wa sekta ya huduma za uzalishaji, biashara ya huduma zilizo na thamani na teknolojia ya juu itaendelea kwa kasi zaidi."

  Bw. Zhu amesema, kuanzia mwezi Januari hadi Aprili mwaka huu, thamani ya biashara ya huduma ya kiujuzi kati ya China na nchi za nje ilizidi dola bilioni 86.7 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 12.7 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, na ongezeko hilo ni kubwa kuliko ongezeko la jumla la biashara ya huduma. Kati ya aina mbalimbali za biashara ya huduma, malipo kwa matumizi ya hakimiliki ya kiubunifu yaliongezeka kwa asilimia 37.8, na mauzo ya huduma za kibiashara kwa nchi za nje yaliongezeka kwa asilimia 21.8. Wakati huohuo, manunulizi ya huduma ya kiujuzi kutoka nchi za nje yalizidi dola bilioni 40.8 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 10.4. Kati ya aina tofauti ya huduma ya kiujuzi, manunulizi ya huduma ya utamaduni na burudani, huduma ya kifedha, na huduma ya upashanaji habari yaliongezeka kwa asilimia 45.2, 42.4 na 30.5.

  Biashara ya huduma ya nje ya China iliongezeka kwa asilimia 2.6 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, na kuongezeka kwa asilimia 4.1 katika miezi minne ya kwanza ya mwaka huu. Bw. Zhu anaona kuwa ongezeko la kasi ya maendeleo ya biashara ya huduma ya nje ya China linaonesha kuwa, China imedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya biashara hiyo.

  Aidha takwimu hizo pia zinaonesha kuwa, katika miezi minne ya kwanza ya mwaka huu, asilimia ya mauzo ya bidhaa za huduma kati ya mauzo ya bidhaa zote ya China kwa nchi za nje imeendelea kuongezeka. Bw. Zhu amesema hali hii inatokana na hatua ya serikali ya kupunguza ushuru na kuhimiza maendeleo ya biashara ya huduma kwa njia ya uvumbuzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako