• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa makala kwenye vyombo vya habari vya Tajikistan

    (GMT+08:00) 2019-06-12 19:40:02

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa makala kwenye vyombo vya habari vya Tajikistan yenye kichwa cha "kushirikiana kujenga ustawi mpya wa urafiki kati ya China na Tajikistan".

    Rais Xi amesema, hali ya usawa na kuaminiana imeufanya urafiki kati ya China na Tajikistan uimarike, na pande mbili zinaelewana, na kuungana mkono katika mambo makubwa yanayohusu maslahi makubwa ya pande mbili. China na Tajikistan zimesonga mbele kwenye ushirikiano wa kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja". China imekuwa nchi iliyowekeza kwa wingi zaidi na mwenzi mkubwa wa biashara wa Tajikistan. Katika miaka kadhaa ijayo, thamani ya biashara kati ya China na Tajikistan itazidi dola za kimarekani bilioni 3.

    Rais Xi pia amesema, tangu Tajikistan iwe nchi mwenyekiti wa mkutano wa hatua za kushirikiana na kuaminiana wa Asia CICA, imetoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya CICA. China inapenda kushirikiana na Tajikistan na nchi nyingine wanachama wa CICA, kuhimiza ushirikiano wa CICA kuingia kwenye kiwango kipya, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa usalama na maendeleo ya Asia na dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako