• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhispania yasema wawekezaji wengi watamiminika Kenya kutokana na hatua za kupiga vita ufisadi

    (GMT+08:00) 2019-06-12 20:13:19

    Taifa la Uhispania limempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa juhudi za kukabiliana na ufisadi na uhalifu wa kiuchumi.

    Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni na Ushirikiano wa Muungano wa Ulaya wa Uhispania,Joseph Borrell Fontelles alimpongeza Rais Kenyatta jana alipomtembelea katika Ikulu ya Nairobi.

    Alisema hatua ya Rais Kenyatta ya kupambana na kumaliza ufisadi itasaidia kuleta imani miongoni mwa wawekezaji kote ulimwenguni.

    Aidha alisema Uhispania iko tayari kushirikia katika mpango wa serikali wa akisema kuwa Uhispania ina kampuni nyingi ambazo zinaweza kuwa washirika wazuri katika ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.

    Utendaji wa jumla wa kiuchumi barani Afrika unaendelea kuimarika na ukuaji wa pato la taifa unatabiriwa kuongezeka hadi asilimia 4.0 mwaka 2019 na asilimia 4.1 mwaka 2020.

    Hayo ni kwa mujibu wa Ripoti ya Kiuchumi Afrika ya mwaka 2019 iliyozinduliwa jana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jijini Malabo,Equatorial Guinea.

    Mkurugenzi wa Utafiti wa AfDB Hnan Morsy alisema utendaji wa jumla wa uchumi barani unaendelea kuimarika,hata hivyo,hali hiyo bado haitoshi kushughulikia changamoto zilizopo za mapungufu ya fedha na madeni mengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako