• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RAGA: Kombe la Elgon- Kenya yabuni mbinu ya kuizamisha Uganda

  (GMT+08:00) 2019-06-13 08:54:58

  Kikosi cha timu ya taifa ya raga ya Kenya (Lionesses) kitakachotegemewa katika kampeni za raga ya wachezaji 15 kila upande mwaka huu kimepunguzwa zaidi na kusalia na wachezaji 40 baada ya mwezi mmoja wa mazoezi.

  Kocha wa timu hiyo Felix Oloo, amekuwa akikinoa kikosi cha wachezaji 50 kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita katika juhudi za kujisuka vilivyo kwa fainali za kombe la Elgon na kampeni za kufuzu kwa kombe la dunia mhcezo wa raga itakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

  Mechi ya mzunguko wa kwanza ya mashindano ya kombe la Elgon itachezwa mjini Kisumu Kenya Juni 22 huku mechi ya marudiano itapigwa jijini Kampala Julai 13.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako