• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa China na Kyrgyzstan wakutana mjini Bishkek

  (GMT+08:00) 2019-06-13 09:19:47

  Rais Xi Jinping wa China jana amewasili Bishkek kwa ziara rasmi nchini Kyrgyzstan, ambapo pia atahudhuria mkutano wa 19 wa Baraza la wakuu wa nchi wanachama wa SCO.

  Baada ya kuwasili Bishkek, rais Xi alikutana na rais Sooronbay Jeenbekov ikulu nchini humo.

  Katika mazungumzo yao, Rais Jeenbekov amesema, Kyrgyzstan inapenda kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana katika nyanja mbalimbali na kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Pia kutumia fursa ya maendeleo ya kasi ya uchumi wa China, kuhimiza maendeleo makubwa ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Kwa upande wake, Rais Xi amesema, tangu China na Kyrgyzstan zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 27 iliyopita, uhusiano huo umeendelezwa vizuri, nchi hizo mbili zimejenga hali ya kuaminiana kisiasa, kushirikiana kiuchumi, kusaidiana kiusalama na kuungana mikono katika jumuiya ya kimataifa. Amesema China inapenda kushirikiana na Kyrgyzstan kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili na kupata matokeo mengi zaidi, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako