• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jimmy Carter apewa tuzo kutokana na mchango wake kwa uhusiano kati ya Marekani na China

  (GMT+08:00) 2019-06-13 17:06:01

  Aliyekuwa rais wa Marekani Jimmy Carter amekuwa kiongozi wa kwanza kupewa tuzo na Mfuko wa uhusiano kati ya Marekani na China wa George Bush wa Marekani inayotolewa kwa viongozi waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani.

  Alipokuwa rais wa Marekani, Bw. Carter ambaye sasa ana umri wa miaka 94, China na Marekani zilianzisha rasmi uhusiano wa kibalozi. Wakati mvutano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili unaongezeka, tuzo hiyo ni pigo kubwa kwa kauli inayosema Marekani na China zinatengana.

  Ziara ya siku saba ya Richard Nixon nchini China "ilibadilisha dunia", Jimmy Carter aliamua kuwa na "mawazo mapya" wa uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, na George Bush alikuwa rais mteule wa Marekani aliyefanya ziara mapema zaidi nchini China. Marais hao wa zamani wa Marekani walichagua kuendeleza uhusiano na China, kwani walitambua kuwa, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kubwa utaleta maendeleo na utulivu wa kikanda na kimataifa, na pia utahakikisha kihalisi maslahi ya Marekani.

  Wakati China na Marekani zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi mwaka 1979, biashara kati ya nchi hizo mbili ilikuwa dola bilioni 2.5 tu za kimarekani, na mwaka jana, biashara hiyo imezidi dola bilioni 630, na kuongezeka kwa mara 252. Aidha, hivi sasa mapato ya makampuni ya Marekani nchini China yanafikia dola bilioni 700 kwa mwaka. Mwaka huu Bw. Carter alisema kuanzisha uhusiano wa kibalozi kati ya Marekani na China ni uamuzi wake mzuri zaidi kwa kuhimiza amani na maelewano duniani.

  Lakini serikali ya sasa ya Marekani imeacha njia iliyochaguliwa na watangulizi wao, na kusababisha hali ya wasiwasi kwa uhusiano kati ya nchi hiyo na China. Kutokana na maendeleo ya kasi ya China, baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanataka "kutenganisha Marekani na China", na kufanya vita baridi na China. Kitendo hicho kinachotaka kufuata matokeo ya ushirikiano kati ya China na Marekani kitadhuru maslahi ya nchi hizo mbili na ustawi na utulivu wa dunia nzima.

  Hivi karibuni, kwenye mkutano wa hadhara, Bw. Carter alisema, rais Donald Trump alimpigia simu na kumwelezea wasiwasi wake kuwa, China itaipita Marekani. Bw. Carter alimjibu rais Trump kwamba, katika miaka mingi iliyopita, Marekani imehangaika na vita, huku China ikijitahidi kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya watu. Alisisitiza kuwa, nchi yenye nguvu ya kupita kiasi si kama tu ni nchi yenye nguvu kubwa zaidi ya kijeshi, bali pia inapaswa kuwa mtangulizi katika kuboresha maisha ya wananchi wake.

  Kama Bw. Carter alivyosema, Marekani na China zina tofauti katika utamaduni, historia, muundo wa serikali, maslahi na kiwango cha maendeleo, na pia zina maoni tofauti kuhusu masuala mbalimbali, lakini nchi hizo zina lengo la pamoja, yaani kuheshimiana, kudumisha amani, ustawi na maendeleo, ambayo ni muhimu zaidi kuliko maoni tofauti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako