• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa India asema kutilia maanani jukumu la Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai

    (GMT+08:00) 2019-06-13 19:12:04

    Waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi amesema India inatilia maanani michango inayyotolewa na Jumuiya ya Ushirikiano la Shanghai (SCO) katika kuhimiza ushirikiano wa pande nyingi za kikanda, siasa, usalama, uchumi, na mawasiliano ya binadamu.

    Bw. Modi amesema hayo kabla ya kuondoka New Delhi na kwenda mjini Bishkek, Kyrgyzstan kuhudhuria mkutano wa kamati ya wakuu ya nchi wanachama wa SCO. Ameongeza kuwa atafanya mkutano wa pande mbili na viongozi wa nchi nyingine za jumuiya hiyo, na kufanya ziara rasmi nchini Kyrgyzstan baada ya mkutano huo, na kushiriki katika mkutano wa mara ya kwanza wa baraza la uchumi kati ya India na Kyrgyzstan. Pia anatumai kuimarisha uhusiano kati ya India na nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako