Mwenyekiti wa Bodi ya TTB, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo alibainisha kuwa kiongozi wa msafara atakuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki.
Alisema ziara hiyo ya wiki moja inaanza Juni 19 hadi 26 katika miji minne ya China ambayo ni Beijing, Shangha, Nanjig, Changsha, lengo likiwa ni kuhakikisha Tanzania inaongeza sehemu ya umiliki wa soko kwenye soko la utalii China.
Alisema katika ziara hiyo TTB itaambatana na wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi na ya umma ikiwamo TANAPA, NCAA, Wakala wa Huduma za Misitu, Makumbusho ya Taifa Idara ya Mambo ya Kale Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Jaji Mihayo alisema Shirika la Utalii Dunia (UNWTO) na vyanzo vingine mbalimbali duniani vimebainisha kuwa soko la watalii kutoka China linaendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watalii na mchango katika uchumi wa dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |