• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima kufaidika na mkopo wa Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2019-06-13 19:40:54
    Umoja wa ulaya umetoa dola milioni 60 za kutoka mikopo kwa wakulima na wasindikaji wa bidhaa za kilimo.

    Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Kenya Walter Tretton amesema fedha hizo zitatolewa ndani ya miaka 7 na zitasimamiwa na benki ya Equity.

    Baadaye Umoja huo pia umetengaza kuwa utatoa dola milioni 10 kwa awamu mbili moja ikiwa kama mkopo kwa benki ya Equity na nyingine kama ruzuku kwa watakaopewa mkopo.

    Wakulima na wajasiriamali wa sekta ya kilimo watakaguliwa upya ili kubaini iwapo wanatimiza viwangi vya kupata mikopo na ruzuku hiyo.

    Msimamizi wa Equity Group Polycarp Igathe amesema fedha hizo zitasaidia wakulima kufikia mahitaji yanayoongezeka na pia kuwaunganisha moja kwa moja na wanunuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako