• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uwekezaji kutoka nje waendelea kuongezeka nchini China

  (GMT+08:00) 2019-06-13 19:47:36

  Takwimu zilizotolewa leo na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, China imetumia kihalisi uwekezaji kutoka nje wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 53.5, ambalo ni ongezeko la asilimia 6.8 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Hali hii inaonesha kuwa China bado inavutia uwekezaji kutoka nje, na kauli ya Marekani ya kusema hatua yake ya kuongeza ushuru wa bidhaa za China inafanya makampuni ya nje yaondoke China haina msingi wowote.

  Madhumuni ya Marekani kutoa kauli hiyo ni kupotosha ukweli ili kuishinikiza China kukubali makubaliano ya biashara yasiyo na haki. Kwa kweli baadhi ya makampuni ya uzalishaji wa bidhaa za kawaida kama nguo yanahamia nchi za kusini mashariki mwa Asia kutoka China, lakini chanzo cha hali hiyo si Marekani, bali ni kuinuka kwa kiwango cha uchumi wa China. Wakati huohuo, makampuni mengi ya teknolojia za juu yanaingia nchini China.

  Takwimu zilizotolewa na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, mwaka jana uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje duniani ulipungua kwa asilimia 9, huku uwekezaji kutoka nje nchini China ukiongezeka kwa asilimia 4.

  Mivutano ya kibiashara iliyoanzishwa na Marekani imeleta hali ya utatanishi kwa uchumi wa dunia, lakini China imethibitisha kuwa nchi ya kuaminika kwa wawekezaji wa kimataifa kwa hatua halisi za kufungua mlango, kulinda maslahi ya wawekezaji kutoka nje, na kuwapatia huduma bora zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako