• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Uganda asema mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani utaathiri ustawi wa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-06-14 09:08:46

    Mwenyekiti wa Shirikisho la vijana la Chama tawala cha Uganda NRM Bw. Nassur Gaddafi amesema, chanzo kikuu cha mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani ni kuwa Marekani imehisi tishio kutokana na maendeleo ya kasi ya China. Anaona, mgogoro huo utaathiri maendeleo na ustawi wa nchi zinazoendelea hasa zile za Afrika, na Marekani inapaswa kuonesha udhati zaidi na kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo.

    Mwenyekiti wa Shirikisho la Vijana la Chama tawala cha Uganda NRM Bw. Nassur Gaddafi anaona kuwa, China na Marekani zikiwa ni nchi mbili zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, mgogoro wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili huwa na athari kubwa zaidi kwa nchi nyingine duniani kuliko kwa nchi hizo zenyewe, haswa zile nchi zinazoendelea zinazonufaika kutokana na uchumi wa nchi hizo mbili. Anasema,

    "Methali ya kiafrika inasema, 'mafahari wawili wakipigana, ziumiazo nyasi.' Kwa hivyo, katika hali hii, nafuatilia kwa karibu mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, kwa kuwa utakuwa na athari hasi kwa ukuaji na ustawi wa Afrika na sehemu nyingine duniani, kwa hivyo tunaona kuwa nchi hizi mbili zinapaswa kurejea kwenye meza ya mazungumzo."

    Akizungumzia chanzo kikuu cha mgogoro huo kati ya China na Marekani, Bw. Gaddafi anaona, Marekani inajaribu kukwamisha maendeleo ya China. Anasema,

    "China imeendelea kwa kasi sana, huenda itakuwa na uchumi mkubwa zaidi duniani, hali ambayo itakuwa ngumu kwa Marekani kuikabili, kwa hivyo wanajaribu kuonesha umwamba na kuchukua hatua za ukandamizaji. Nchi nyingi za magharibi zinaogopa kuibuka kwa China, lakini naona wanapaswa kuukabili mwelekeo huu, kwa kuwa maendeleo ya China sio muundo mbaya, na China pia sio mshirika mbaya wa ushirikiano, China ni nchi inayofungua mlango kwa nje. Niliwahi kutafiti historia ya China, China inafungua mlango wake kwa dunia nzima."

    China imekuwa mshirika mkubwa wa kwanza wa biashara wa Afrika kwa miaka mingi mfululizo. Bw. Gaddafi anaona, Uganda ina miundombinu dhaifu, China imeisaidia Uganda kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara na vituo vya umeme, na kutoa misaada mingi kwa Uganda kila mwaka, kwa hivyo wanaihitaji China.

    Ofisa huyo pia amesema, ana imani kuwa China itasimama hadi mwisho, na Marekani inapaswa kuonesha udhati zaidi. Anaona hatua za upande mmoja zinaharibu uchumi wa dunia, na anaamini kuwa biashara kati ya China na Marekani inaweza kufanyika kwa njia ya kirafiki, na inahitaji juhudi za pamoja za nchi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako