• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ratiba ya ligi kuu Uingereza yatoka, mechi zitaanza Ijumaa Agosti 9

    (GMT+08:00) 2019-06-14 09:11:27

    Baada ya ligi mbalimbali duniani kumalizika na kila ligi kujulikana bingwa, Uingereza bingwa alikuwa Manchester City, Uhispania bingwa Barcelona, Ujerumani Bingwa Bayern Munich na ufaransa bingwa akiwa PSG lakini nchini Italia bingwa akiwa Juventus.

    Tayari msimu 2019/2020 unatarajiwa kuanza mapema mwezi wa 8 na ligi ya Uingereza wametangaza tarehe rasmi ya ligi hiyo kuanza.

    Liverpool itaanza na Norwich, huku mashetani wekundu Manchester United watawakaribisha watoto wa darajani Stamford Chelsea katika dimba la Old Traford, huku West Ham wao watamenyana na Manchester City, AFC Bournemouth watakutana na Sheffield United, Burnley watamenyana na Southampton, huku Wolves uso kwa uso na Leicester City, Tottenham Hotspurs itawakabili Aston Villa, na Watford dhidi ya Brighton, huku Crystal Palace wao watakutana na Everton, na Newcastle watawakaribisha washika bunduki wa njiji la London Arsenal.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako