• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Iran wakutana

    (GMT+08:00) 2019-06-14 19:07:43

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Iran Bw. Hassan Rouhani mjini Bishkek nchini Kyrgyzstan.

    Rais Xi amesema China inaunga mkono kulinda makubaliano yaliyofikiwa kuhusu suala laa nyuklia la Iran, na ina nia ya kuimarisha uratibu katika mifumo ya pande nyingi ikiwemo Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Pia inapenda kulinda kwa pamoja kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea ikiwemo China na Iran.

    Rais Rouhani amesema, uhusiano kati ya Iran na China ni wa kimkakati na wa muda mrefu, na Iran inatilia maanani kuendeleza uhusiano kati yake na China na kushiriki katika kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja," na kuongeza uwezo wa ushirikiano wa sekta mbalimbali kati ya pande hizo mbili. Amesema Iran inasifu juhudi za China katika mambo ya kimataifa na ina nia ya kuimarisha mawasiliano na uratibu na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako