• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Zimbabwe aipongeza kampuni ya China kwa kufikia hatua nzuri kwenye ujenzi wa jengo jipya la bunge

  (GMT+08:00) 2019-06-14 20:47:00

  Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametembelea jengo jipya la Bunge linalojengwa na kampuni ya ujenzi ya China ya Shanghai Construction Group, na kueleza kuridhishwa na hatua nzuri iliyofikiwa hadi sasa.

  Rais Mnangagwa ameyaeleza hayo jana baada ya kutembelea mradi huo na kusisitiza kwamba amefurahia kuwa ujenzi huo unaendelea na hadi sasa hakuna tukio lolote lililotokea, pia amesema anatarajia rikodi hiyo nzuri itaendelea hadi kukamilika kwa mradi huo. Rais huyo amesema Zimbabwe inaishukuru China kwa kuipa ruzuku kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la Mt Hampden kwenye viunga vya Harare, na eneo la mji mpya wa satelite karibu na mji mkuu.

  Kwa mujibu wa kampuni ya ukandarasi, mradi huo uko mbele ya ratiba kwa wiki na hautaathirika na tatizo la ukatikaji umeme linaloathiri taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako