• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UHAMISHO: Maurizio Sarri asema byebye kwa Klabu ya Chelsea na kuhamia klabu ya Juventus ya Italia

  (GMT+08:00) 2019-06-17 08:29:39

  Klabu ya Chelsea ya England jana ilitangaza rasmi kuwa aliyekuwa kocha wao Maurizio Sarri kaihama klabu hiyo na kujiunga na club ya Juventus ya Italia, Sarri anarudi Italia kujiunga na Juventus kwa mkataba wa miaka mitatu, hiyo ni baada ya kuifundisha Chelsea kwa msimu mmoja pekee. Kocha Maurizio Sarri amejiunga na Juventus akitokea Chelsea, Sarri anaondoka Chelsea akiwa kaisaidia kutwaa taji moja la UEFA Europa League 2018/19 na kuvunja rekodi yake ya kukaa miaka 11 bila taji lolote akiwa kafundisha vilabu 7. Moja ya sifa ambazo Chelsea watamkumbuka Sarri ni pamoja na kuisaidia timu hiyo kupata nafasi ya kucheza UEFA Champions League kwa msimu wa 2019/2020, hata hivyo aliifikisha pia Chelsea fainali ya Capital One Cup na kupoteza mchezo huo kwa kufungwa na Man City.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako