• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikundi cha Bibi Tu Youyou chatatua tatizo la usugu wa vimelea vya malaria dhidi ya dawa ya artemisinin

    (GMT+08:00) 2019-06-17 16:54:01

    Mshindi wa tuzo ya Nobel Bibi Tu Youyou amesema kikundi chake kimependekeza njia za kutatua tatizo la usugu wa vimelea vya malaria dhidi ya dawa ya artemisinin, na kutoa ushahidi mpya kuwa artemisinin ni dawa namba moja duniani kwenye kupambana na malaria.

    Kikundi cha Bibi Tu Youyou kimekuwa kinafanya utafiti kuhusu usugu tangu mwaka 2015, na kugundua kuwa sehemu ya usugu huo inatokana na kuchelewa kwa vimelea vya malaria kutoka kwenye mkondo wa damu, kutokana na matumizi ya tiba mseto.

    Bibi Tu Youyou amesema vimelea vinaweza kulala katika siku tatu za matumizi ya dawa mseto ya artemisinin, lakini dawa hiyo ikitumiwa kwa siku tano hadi saba, usugu unaweza kuondoka na vimelea vinakufa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako