• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yashauriwa itangaze masoko ya madini nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2019-06-18 19:25:28

    Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji madini Mkoa wa Manyara ,Justine Nyari ameishauri Wizara ya Madini kuyatangaza nje ya nchi masoko ya madini yanayofunguliwa katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.

    Nyari aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa soko la madini la kimataifa la Arusha.

    Aidha alitaja wanunuzi wakubwa wa vito vikiwamo Tanzanite kuwa ni pamoja na Marekani,Ujerumani,China na Hongkong.

    Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,aliiomba Wizara ya Madini kuuruhusu mkoa huo kuendelea kufanya maonyesho ya madini ya kimataifa kutokana na kuwa kitovu cha biashara nchini Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako