• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yaweka vigezo tofauti katika ulinzi wa hakimliki

  (GMT+08:00) 2019-06-19 10:10:45

  Mbunge wa baraza la seneti la bunge la Marekani Marco Rubio ametoa mswada wa kusahihisha sheria ya ulinzi, kwa kulenga kupiga marufuku Kampuni ya Huawei ya China kudai malipo ya hataza kwa makampuni ya Marekani.

  Habari hii imewashangaza watu wa dunia nzima wakiwemo wamarekani, kwani kwa upande mmoja Marekani inayataka makampuni ya nchi za nje kulipa malipo ya hataza kwa makampuni yake, kwa upande mwingine nchi hiyo inapiga marufuku makampuni ya nchi nyingine kudai malipo ya hataza kwa makampuni yake, kitendo ambacho ni sawa na uporaji.

  Mara kwa mara Rubio anailaani China kwa "kuiba hakimiliki bunifu za makampuni ya Marekani". Wakati kampuni ya Huawei inapotaka Shirika la Habari na Mawasiliano ya Simu za Mkononi la Verizon la Marekani liilipe dola bilioni moja za kimarekani kutokana na matumizi ya hataza za Huawei, Rubio anasahau nia yake ya kulinda hakimiliki za kiubunifu, na kusema Huawei ni "mhuni wa hataza", na kujaribu kupiga marufuku malipo hayo kwa kurekebisha sheria.

  Inaonekana kuwa, kwa wanasiasa wa Marekani kama Rubio, kulinda hakimiliki za kiubunifu ni moja ya nyenzo ya kisiasa ambayo wanaweza kuitumia wanavyopenda. Lakini kitendo cha Rubio kimewatambulisha watu duniani kuwa, Marekani inaweka vigezo tofauti katika kulinda hakimiliki za kiubunifu.

  Tangu Rubio achaguliwe kuwa seneta mwaka 2011, ameonesha uhasama mkubwa dhidi ya China. Alihimiza baraza la chini la bunge la Marekani kupitisha "sheria ya safari katika sehemu ya Taiwan", kutetea kupiga marufuku idara za serikali ya Marekani kuagiza vifaa vilivyotengenezwa na China, kutaka kuiondoa Taasisi ya Confucius ya China nchini Marekani, na kulaani hali ya haki za binadamu nchini China.

  Mwaka 2016, Rubio aligombea urais, lakini alishindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa wateule wa Chama cha Democratic, lakini hakukubali kushindwa, na mara kwa mara alitoa miswada dhidi ya China ili aonekane kuwa "mzalendo".

  Lakini ukweli ni kwamba, Rubio anaidhuru Marekani kwa kisingizio cha uzalendo, na kuharibu maslahi ya watu wa nchi hiyo kwa ajili ya maslahi yake binafsi ya kisiasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako