Wataalamu na watunga sera wa Afrika wamehimiza juhudi za pamoja kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa nishati, na kutoa mwito wa uwekezaji zaidi kwenye sekta ya nishati endelevu.
Wito huo umetolewa kwenye Mkutano wa nishati endelevu wa Afrika uliofanyika jana mjini Addis Ababa, Ethiopia, ukiwa na kaulimbinu ya "Kuziba Pengo la Upatikanaji wa Nishati Barani Afrika".
Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa ECA Bi. Vera Songwe amezihimiza nchi za Afrika na washirika wao wa maendeleo kutatua changamoto za nishati zinazoikabili Afrika kwa "ajenda ya dharura na yenye malengo makuu".
Bi. Songwe amesema Afrika itashuhudia ongezeko kubwa la mahitaji ya nishati kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, kupanuka kwa tabaka la kati, maendeleo ya viwanda, mabadiliko ya tabianchi, uendelezaji wa miji na kuanzishwa kwa Eneo la Biashara Huria la Afrika AfCFTA.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |