• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uagizaji wa nguo kuukuu nchini Uganda waongezeka

    (GMT+08:00) 2019-06-20 18:37:42
    Uagizaji wa nguo kuukuu nchini Uganda umeongezeka kwa mara tano kutoka dola milioni 27 mwaka 2001 hadi dola milioni 137 mwaka 2016.

    Ripoti ya kituo cha utafiti wa sera za kiuchumi inasema uagizaji wa nguo mpya nao umefikia dola milioni 83 ndani ya kipindi hicho.

    Imesema uagizaji wa nguo kwa wingi umechangiwa na kuongezeka kwa idadi ya watu na kupungua kwa uwezo wa viwanda vya ndani wa kuzalisha.

    Uagizaji wa nguo kuukuu na mpya umekuwa na mjadala mkali wanaoupinga wakisema unapunja viwanda vya ndani, sekta ya kilimo na kuchangia kupotea kwa ajira.

    Mwaka 2016 nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, na Burundi ziliweka mpango wa miaka 3 wa kupiga marufuku uagizaji wa nguo kuukuu huku kanda hiyo ikielekea uchumi wa kujitegemea kiviwanda 2050.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako