• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China kuhudhuria mkutano wa Kundi la Nchi 20

  (GMT+08:00) 2019-06-24 16:55:14

  Rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 14 wa kilele wa kundi la nchi 20 (G20) kuanzia tarehe 27 hadi 29 utakaofanyika mjini Osaka, Japan. Hii itakuwa mara ya saba mfululizo ya rais Xi kuhudhuria mkutano huo.

  Mratibu wa mambo ya G20 wa China, ambaye pia ni msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zhang Jun amewaambia waandishi wa habari kuwa, rais Xi atahuhuria vikao vinne vya wajumbe wote wa mkutano huo kuhusu masuala ya uchumi na biashara, uchumi wa kidigitali, maendeleo endelevu na shirikishi, miundombinu, mabadiliko ya hali ya hewa, nishati na uhifadhi wa mazingira, na kufafanua msimamo wa China kwa kina.

  Hivi sasa, vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara vinaharibu utaratibu wa uchumi wa dunia, na hali ya hatari na utatanishi inaongezeka. Ukiwa mkutano muhimu wa ushirikiano wa uchumi duniani, mkutano huo unafuatiliwa na pande mbalimbali. Bw. Zhang amesema China inapenda kuhimiza mkutano huo kupata matokeo chanya. Anasema,

  "Tunapenda kulinda utaratibu wa pande nyingi kwa kushirikiana na nchi nyingine. Kutokana na hali ya hivi sasa, Kundi la Nchi 20 linapaswa kuonesha msimamo wazi wa kulinda utaratibu huo, kulinda sheria na haki ya kimataifa, na kurejesha uchumi wa dunia kwenye njia sahihi ya maendeleo."

  Takwimu zilizotolewa na Shirika la Biashara Duniani zinaonesha kuwa, kiwango cha ustawi wa biashara ya kimataifa duniani kwa robo ya pili ya mwaka huu ni 96.3, na ni cha chini zaidi tangu mwezi Machi mwaka 2010. Wakati huohuo, ripoti iliyotolewa na mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa, mwaka jana uwekezaji wa kimataifa wa moja kwa moja ulipungua kwa asilimia 13. Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Shouwen anasema,

  "Kuna nchi inayofanya vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara, kutumia vibaya sheria ya usalama wa ndani, na kuongeza ushuru wa bidhaa kutoka wenza wake wa kibiashara. Hali hii imeleta tishio kubwa kwa ongezeko la uwekezaji na uchumi duniani. Nchi wanachama wa G20 zina majukumu na uwezo wa kuchukua hatua ya pamoja kulinda utaratibu wa pande nyingi na biashara huria."

  Aidha, kwenye mkutano huo, rais Xi pia atafanya mazungumzo yasiyo rasmi na viongozi wa Kundi la BRICS, Russia na Afrika, ili kubadilishana maoni na kuongeza uratibu kuhusu masuala muhimu yakiwemo kukuza ushirikiano kati ya nchi zinaoibuka kiuchumi na nchi zinazoendelea, na kutekeleza ajenda ya maendeleo ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa. rais Xi pia anatarajiwa kukutana na viongozi wa nchi ningine watakaohudhuria mkutano huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako