• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Qishan akutana na ujumbe wa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-06-24 19:05:35

    Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan leo amekutana na viongozi wa ujumbe wa Afrika wa mkutano wa wasimamizi wa utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushrikiano kati ya China na Afrika FOCAC kwa pamoja kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Umma wa China.

    Bw. Wang Qishan amesema kutokana na juhudi za viongozi na watu wa China na Afrika, uhusiano kati ya China na Afrika umeendelea vizuri na kupata mafanikio makubwa. Amesema kufanya mkutano wa wasimamizi wa utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa Beijing wa wakuu wa FOCAC uliofanyika mwezi Septemba mwaka jana, ni hatua muhimu ya ushirikiano kati ya China na Afrika kutekeleza matokeo hayo na pia ni jambo kubwa katika uhusiano kati ya pande hizo mbili kwa mwaka huu. Amesema China itaendelea kushirikiana na Afrika kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Afrika, na kujenga jumuiya yenye mustakbali wa pamoja ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako