• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais kuwekeza kwa kiwanda cha nguo Rivatex kuunda kazi zaidi ya 3,000

    (GMT+08:00) 2019-06-24 20:18:56

    Rais Uhuru Kenyatta alitimiza mojawapo ya ahadi zake za kampeni za uchaguzi, Ijumaa wakati alipomaliza kufanyia ukarabati kiwanda cha nguo cha Rivatex katika mji wa Eldoret.

    Kiwanda kipya ambacho kilifanyiwa ukarabati kwa gharama y ash bilioni 5, kitafungua nafasi za ajira zaidi ya 3,000 mpya, kupiga jeki uchumi wa mji wa Eldoret pamoja na kubadilisha miasha ya maelfu ya wakulima wa pamba katika kaunti zaidi ya 24 nchini kote.

    Ili kushawishi kiwanda cha Rivatex katika kutengeneza faida, Rais ametangaza kuwa serikali itaongeza usambazaji wa nguvu za umeme kutoka 33 KVA hadi 66 KVA ili kuwezesha kiwanda cha nguo kufanya kazi kwa saa 24.

    Aidha aliagiza Wizara ya Nishati kupunguza bei ya umeme iliyotumika kwa kiwanda kwa asilimia 50.

    Pia Aliwahimiza Wakenya wote, sana sana vijana, kukubali kuvaa nguo zilizotengenezwa humu nchini ili kusaidia sekta ya nguo kukua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako