• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AFCON: Kodjia aitoa kifua mbele Ivory Coast dhidi ya Afrika Kusini

  (GMT+08:00) 2019-06-25 08:33:50

  Katika kindumbwendubwe cha Afcon jana mshambuliaji wa Aston Villa Jonathan Kodjia amefunga goli pekee liloamua mchezo baina ya Ivory Coast na Afrika Kusini. Mchezaji huyo aliunganisha pasi safi kutoka kwa Max Gradel kwa kupiga shuti fupi lilomshinda kipa wa Afrika Kusini Ronwen Williams katika dakika ya 64. Mshambuliaji mwengine hatari wa Ivory Coast, Nicolas Pepe 23, aligongesha mwamba kipindi cha kwanza, na shuti lake la mkwaju wa faulo kuokolewa na Williams kipindi cha pili. Huu ni mchezo wa pili wa kundi D, jana Jumapili Morocco iliifunga Namibia 1-0. Ivory Coast - ambayo ilianza bila mshambuliaji machachari wa klabu ya Crystal ya England Wilfried Zaha - waliutawala vyema mchezo huo katika kipindi cha kwanza wakienda mapumziko bila kupata goli. Hlatswayo aliikosesha Afrika Kusini ama Bafana Bafana goli la wazi kwa kupaisha kichwa krosi safi kutoka kwa Sifiso Hlanti.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako