Wakenya Fancy Chemutai na David Bett wameibuka mabingwa wa mbio za kilomita 10 za Boston (B.A.A. 10k) nchini Marekani mnamo Juni 23, 2019. Chemutai na Bett, ambao wamejizolea Sh1 milioni kila mmoja, wamekata utepe kwa kukamilisha umbali huo kwa dakika 30:36 na 28:08, mtawalia. Chemutai alivunja rekodi ya B.A.A. 10k iliyowekwa na Mmarekani Shalane Flanagan mwaka 2016 kwa sekunde 16. Chemutai, ambaye ni mkimbiaji aliye na kasi ya tatu-bora duniani katika kilomita 10, alifuatwa kwa karibu na Wakenya wenzake Brilliant Kipkoech (31:04) na Caroline Rotich (31:58). Katika kitengo cha wanaume, Bett alifuatwa sekunde moja nyuma na Mkenya Daneil Chebii, huku Mkenya mwingine Stephen Sambu akifunga mduara wa tatu-bora kwa dakika 28:11.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |