• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa waratibu wa kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC wafanyika

    (GMT+08:00) 2019-06-25 16:30:16

    Mkutano wa waratibu wa kutekeleza matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC umefanyika leo hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za kupongeza mkutano huo, akitaka China na Afrika zichukue mkutano huo kama fursa mpya ya kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuboresha maisha ya watu bilioni 2.6 wa China na Afrika, na kujitahidi kujenga jumuiya ya China na Afrika iliyo karibu zaidi na yenye mustakabali wa pamoja.

    Kwenye salamu zake, rais Xi amesisitiza kuwa, hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita, na nchi zinazoendelea zimepata maendeleo ya kasi. Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika kwa ajili ya maendeleo ya pamoja utatoa mchango muhimu kwa ongezeko la nguvu ya nchi zinazoendelea na ujenzi wa uhusiano mpya wa kimataifa na jumuiya yenye muskatabali wa pamoja.

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi akihutubia ufunguzi wa mkutano huo amesema, China siku zote inatilia maanani na kuheshimu Afrika, na imepata njia ya kushirikiana na Afrika ambayo ni tofauti na zile za nchi nyingine kubwa. Anasema,

    "Baadhi ya nchi zinapaka matope ushirikiano kati ya China na Afrika, na kutunga uvumi wa "ukoloni wa mambo leo", na "mtego wa madeni". Uvumi huo haulinganishi na hali halisi, na haukubaliwi na watu wa Afrika."

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ambaye ni mgeni maalumu wa mkutano huo amesema, hivi sasa nchi mbalimbali za Afrika zinakabiliwa na changamoto katika ngazi tofauti, "hatua nane" za ushirikiano kati ya China na Afrika zilizotolewa na rais Xi zinalingana na mahitaji ya Afrika katika mchakato wa maendeleo, na zitasaidia bara hilo kutatua masuala magumu ya maendeleo. Anasema,

    "Afrika na China zinapaswa kupendekeza kujenga mfumo wenye usawa wa amani na maendeleo, na kuwezesha binadamu waache mawazo ya kuvutana kimaslahi, na kujitahidi kwa pamoja kupata mafanikio ya pamoja."

    Waziri wa mambo ya nje wa Senegal ambaye ni nchi mwenyekiti wa Afrika katika mkutano huo Bw. Amadou Ba amesema, FOCAC ni mali ya pamoja ya Afrika na China, na italeta maisha bora kwa watu wa pande hizo mbili. Afrika na China zinapaswa kusukuma mbele kithabiti ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja. Anasema,

    "Hivi sasa utaratibu wa kimataifa na mfumo wa pande nyingi unakabiliwa na changamoto. Tunapaswa kushikamana zaidi, kuimarisha ushirikiano wetu na kuhimiza utaratibu wa kimataifa uelekee kuwa shirikishi na wa haki zaidi, na kuzingatia malengo ya ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja. Hivyo tutaleta fursa zaidi kwa watu na nchi yetu."

    Mkutano wa waratibu wa kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC umefanyika tarehe 24 na 25 hapa Beijing, na kuhudhuriwa na mawaziri wa China na nchi 54 za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako