• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya FedEx yaishitaki wizara ya biashara ya Marekani kwa kuweka vizuizi dhidi ya kampuni ya Huawei

  (GMT+08:00) 2019-06-25 18:39:45

  Kampuni ya kusafirisha vifurushi ya Marekani FedEx imeifungulia mashtaka wizara ya biashara ya Marekani kuhusiana agizo la kuitaka kampuni hiyo iweke vizuizi dhidi ya kampuni ya Huawei.

  Wizara ya biashara ya Marekani ilifikia uamuzi huo baada ya rais Donald Trump kutoa agizo la dharura kwa kile alichokiita hatari kwa teknolojia za Marekani.

  Kwenye mashtaka hayo yaliyofunguliwa kwenye mahakama katika wilaya ya Columbia, kampuni ya FedEx inasema hatua ya wizara hiyo inaweka mzigo usio wa lazima kwa kampuni ya FedEx kukagua mamilioni ya vifurushi kwenye mtandao wake kila siku. Kampuni hiyo imesema serikali ya Marekani imetoa agizo ambalo linakiuka haki za kikatiba za kampuni hiyo, na ambalo ni vigumu kutekeleza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako